Yaliyojiri

 #HABARI: Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini imemfikisha Mahakamani Abuu Hemed Mbaga kwa tuhuma za kusafirisha kilogramu 134.5 za dawa za kulevya aina ya mirungi. 


Kesi hiyo, namba 4368/2026, ilisomwa mbele ya Mheshimiwa Mhenga katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi, ikimhusisha pia Aminiel Lenard Mvungi aliyekamatwa katika Kijiji cha Kahe mkoani Kilimanjaro.


Kutokana na kosa hilo kutokuwa na dhamana, mtuhumiwa amepelekwa katika Gereza la Karanga kusubiri hatua zaidi za kisheria. 


Kesi hiyo imepangwa kutajwa tena mahakamani hapo Machi 11, 2026, huku mamlaka ikiendelea na jitihada za kudhibiti biashara haramu ya dawa za kulevya katika kanda hiyo ya kaskazini.


Powered by #rbc updates 


rbcdailyupdatestz.blogspot.com 

Follow for more breaking news 




Maoni

Machapisho Maarufu